Katika Eneo la Adui Kuokolewa na Silaha ya Siri: Swahili Katika Eneo la Adui Kuokolewa na Silaha ya Siri: Swahili

Katika Eneo la Adui Kuokolewa na Silaha ya Siri: Swahili

    • 6,99 €
    • 6,99 €

Publisher Description

Ili kuendelea kuishi nchini Vietnam, ili uweze kurudi nyumbani ukiwa mzima, unahitajika kupitia mafundisho ya hali ya juu, kupata ozoefu wa mwili na akili na kuwa na uhusiano mwema na wenzako. Kama tungeshindwa kuwa makini, kutotii, kupuuza, au kutozingatia nia yetu kuu mahali pale, basi idadi ya kuishi ilipungua kwa kiasi kikubwa.

Niamini nikisema, kuna mambo mengi yalituzuia. Baadhi yetu tulianza kutumia madawa ya kulevya, unywaji wa pombe, kushiriki ngono kihorera, haya yote katika harakati ya kutafuta maisha ya kupendeza, hatari nyingine ilikua inatukondolea macho, hata kabla twende vitani kupigana na makali ya adui zetu, kabla tuwapate nyoka, magonjwa, na wanyama wa pori walioishi katika maeneo haya

Kitabu hiki kinaelezea matukio ya kusisimua ambayo nilipitia mimi mwenyewe, mafunzo niliyopata, nilivyopata uzoefu na kuwa na uhusiano mwema na wenzangu, nikiwa mwanajeshi wa Marekani katika kikosi cha 75 cha wanahewa wa kupiga doria mnamo mwaka wa 1969 na 1970, tukifanya upelelezi katika maeneo ya adui zetu.

Ni mwaka wa 1971, nikihudumu kama mshauri wa washika doria wa kikosi cha pili milimani, ndani ya msitu katika eneo lililopakana na kambi ya sita katika kijiji cha Plei Mrong, Kusini mwa Vietnam kupakana na nchi ya Cambodia. Jukumu langu lilikuwa kufundisha kikosi cha Mountain Yard na wanajeshi wa Vietnam kuhusu mbinu za kivita na jinsi ya kuwahamisha wanakijiji walioathiriwa na vita.

Matukio haya yatakutoa katika vita vya kimwili nchini Vietnam hadi kwenye vita vya kiroho vinavyoendelea kila siku kwa ajili yako. Maswali mengi kuhusu ulimwengu wa kiroho yatapata majibu na imani yako itachukua mwelekeo mpya. Ombi langu ni kwamba, kupitia kitabu hiki, utapata mtazamo mpya kuhusu vita vinavyoendelea kila siku kati ya wema (Mungu) na ubaya (Shetani) kwa ajili ya nafsi yako, wewe binafsi.
Kwa hivyo tulia na ufurahie kisa hiki kifupi, ingawa kina uzito wake. Lengo langu ni kuwa ukimaliza kukisoma kitabu hiki, utakuwa umemfahamu kabisa mshindi wa Medali ya Heshima ambaye ni Mwokozi Yesu Kristo. Yesu anakupenda na anataka kuwa na uhusiano mwema na wewe, uhusiano utakao leta mabadiliko kwa nafsi yako, kutoka kiumbe ulicho sasa hadi kiumbe kipya. Roho yako ndio msingi wa kitabu hiki.
Mwandishi Danny Clifford

GENRE
Fiction & Literature
RELEASED
2014
2 November
LANGUAGE
SW
Swahili
LENGTH
43
Pages
PUBLISHER
Danny Clifford
SIZE
719.7
KB

More Books by Danny Clifford

Enter Through The Narrow Gate Enter Through The Narrow Gate
2021
Enter Through The Narrow Gate Enter Through The Narrow Gate
2021
Enter Through The Narrow Gate Enter Through The Narrow Gate
2021
Lost Behind Enemy Lines Lost Behind Enemy Lines
2016
Who Do People Say I Am Who Do People Say I Am
2015
Who Do You Say I Am Who Do You Say I Am
2015