Sadaka Ya Tarehe Tano: Msumeno Ulao Mbele Na Nyuma
-
- €1.99
-
- €1.99
Publisher Description
Sadaka ya Tarehe Tano ni Agizo la Agano. Ni msumeno ulao mbele na nyuma; ni dawa na ni sumu; inaweza kuhuisha na inaweza kufisha. Kutotoa Sadaka ya Tarehe Tano ni kukaidi na kukaidi ni dhambi. kKama umekosa, Mungu Anajua huna. Hivyo, hutakuwa na dhambi kwa kutotoa.
Kumbuka u katika Agano ambalo ni makubaliano kati yako na Mungu wako. Hali iliyokufanya ujiunge na Agano la Baba Mtume Elijah liwe ndilo shinikizo lako kutenda la yakupasayo.
Hadithi ya Anania na mkewe Safira inawaumia makuhani na makarani katika Sadaka ya Tarehe Tano. Wenye bahati hutambua wakatubu na kuishi. Wengine hawapewi nafasi. Ya kuwapata huwapata wakawa wa kufahamu baada ya kwenda zao.
Ole wao wailayo Sadaka ya Tarehe Tano,
Ole wao wajikatiao kipande cha Sadaka ya Tarehe Tano,
Ole wao waongeao vibaya kuhusu Sadaka ya Tarehe Tano,
Ole wao wasiojua chochote kuhusu Sadaka ya Tarehe Tano,
Ya kuwapata yatawapata pasipo kujua,
Ila yatasemwa wao wakiozeana udongoni.