Mwongozo wa Kigogo: Maswali na Majibu Mwongozo wa Kigogo: Maswali na Majibu

Mwongozo wa Kigogo: Maswali na Majibu

    • $3.99
    • $3.99

Publisher Description

Mwongozo wa Kigogo ni kitabu ambacho kimetayarishwa kimaksudi kwa lengo la kumsaidia mwanafunzi, mwalimu na msomi wa fasihi katika kuelewa na kuchambua kwa kina tamthlia ya Kigogo. Mwongozo huu una sehemu tatu kuu. Kwanza, ni sehemu inayoshughulikia mtitiriko wa matukio katika kila onyesho na tendo. Sehemu ya pili inazamia uchambuzi wa fani na maudhui nayo ile ya tatu ni sehemu ya kujitathmini. Sehemu hii ya tatu inajumuisha maswali kadha pamoja na majibu yake. Vipengelele vyote vikuu vya uchambuzi wa tamthlia vimeshughulikiwa kwa mapana. Vipengele hivi ni pamoja na: dhamira, maudhui mbalimbali, mbinu za kisanaa pamoja na tamathali za usemi, mandhari, sifa za wahusika na uhusika wao. Ili kumpa msomaji uhondo kamili, maswali kielelezo yametolewa. Haya ni maswali pamoja na majibu yanayolenga kutoa dira ya namna maswali yanavyofaa kujibiwa na uhakiki kutekelezwa. Kila jibu limetolewa hoja za kuridhisha kuambatana na mitindo mipya ya utahini pamoja na matarajio ya watahini. Ni maswali ya kumfikirisha msomaji na wakati huo huo kumpa nyenzo za kukabiliana na maswali mengine. Kuna maswali chungu nzima yakiwa ni pamoja na yale ya dondoo, ya kujadili pamoja na yale ya kuthibitisha kauli na madai yaliyotolewa katika tamthlia. Ni mwongozo ambao umesukwa ukasukika; ukapikwa ukaiva.

GENRE
Reference
RELEASED
2021
31 March
LANGUAGE
SW
Swahili
LENGTH
57
Pages
PUBLISHER
SHADRACK KIRIMI
SELLER
Draft2Digital, LLC
SIZE
160.8
KB

More Books by SHADRACK KIRIMI

Mwongozo wa Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyinginge Mwongozo wa Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyinginge
2021
Mwongozo wa Chozi la Heri: Maswali na Majibu Mwongozo wa Chozi la Heri: Maswali na Majibu
2021