Maono Niliyoona Maono Niliyoona

Descripción editorial

Maono-1(TETEMEKO NA VOLKANO)
Mwaka 2017, niliona maono ya kutisha. Maono yalianza kama ndoto wakati nimelala kitandani na nilipoamka bado maono hayo yaliendelea nikiwa macho na akili zangu timamu. Katika maono hayo niliona kama mlipuko wa volkano kubwa iliyochanganyikana na tetemeko ndani yake. Niliona watu na milima wakiinuliwa juu na kurudishwa chini kiasi cha kutengeneza mzunguko kama vile mtu anavyopatwa na kizungunguzu baada ya kujizungusha kwa muda mrefu. Maono hayo yalikuwa juu ya anga nilipokuwa nimelala kifudifudi nikiangalia kama sinema. Baadae katika maono hayo niliona kama watu wanapigana ndani ya huo mzunguko wa volcano. Wakati naangalia sana, maono yalifika mwisho wake.

Maono-2(KUPANDA MILIMA NA KUSHUKA MABONDE)
Katika maono ya kupanda vilima, nilijikuta napanda jabali lenye ukingo mkali sana unaotisha sana na kuogopesha sana. Wakati napanda kilima hicho nilikuwa peke yangu bila msaada wa mtu. Nilitumia nguvu nyingi na maarifa katika kupanda kilima hicho na baadae nilifanikiwa baada ya kuhangaika na kutumia nguvu kubwa sana.Wakati natafakari maono hayo nilipata ujumbe kuwa kuna nyakati ngumu na majaribu zinakuja mbeleni. Nakumbuka ilinitokea mfululizo zaidi ya mara tano, kuona maono ya kupanda vilima na kuvuka mito yenye kingo ndefu sana. Kupanda vilima na vigongo ilimaanisha nyakati ngumu za kujaribiwa binadamu na kubadilika kwa kawaida ya Maisha ya binadamu. Katika maoni hayo Mungu alikuwa ananionya kuwa Mungu anaenda kuchuja wamwabuduo Mungu kwa dhati na watu wanamtafuta Mungu ili kujipatia faida.Katika maono ya pili tulikuwa tunakimbia kama mashinndano ya watu wasiopungua watano. Maono hayo nakumbuka yalijirudia mara nyingi kidogo kwa siku tofautofauti. Tulikuwa kunakimbia nyikani sehemu ambayo haina watu bali kuna nyika, miiba, vichaka na vikwazo vingi sana. Katika kukimbia tulikutana na mito yenye kina kirefu ila haina maji. Mito hiyo ilikuwa na vikwazo sana kama mizizi ya miti mikubwa, matawi ya miti na zaidi ya yote ukingo wa mto ulikuliwa mrefu sana kiasi cha kutatiza namna ya kupanda ili kuendelea na mashindano yetu. Wakati najaribu kuvuka vikwazo hivyo nilijikuta wenzangu wamenicha nyuma. Nilipomuuliza Mungu kuhusu maono hayo alinifunulia kuwa wakati unakuja kila mtu atasimama katika zamu yake na kujaribiwa imani yake mbele za Mungu.

Maono haya na mengine yalinisukuma kuandika kitabu ili watu wajue mambo yaliyokusudiwa na yale yatakayokuja na namna ya kukabiliana nayo.

GÉNERO
Religión y espiritualidad
PUBLICADO
2020
19 de mayo
IDIOMA
SW
Suajili
EXTENSIÓN
58
Páginas
EDITORIAL
Charles Nakembetwa Shamsulla
VENDEDOR
Draft2Digital, LLC
TAMAÑO
139.2
KB

Más libros de Charles Nakembetwa Shamsulla

The Power of Lending and Borrowing The Power of Lending and Borrowing
2021
Siri ya Dhabihu Siri ya Dhabihu
2020
In the Offering Basket of Jesus In the Offering Basket of Jesus
2020
The Lord Appeared to Me The Lord Appeared to Me
2020
You Can Conquer ALL Diseases You Can Conquer ALL Diseases
2020
Steps to Child Care Steps to Child Care
2017